→ Mellania Julius Mkundi
→ Menu

Mellania Julius Mkundi

Mellania Julius Mkundi alizaliwa mwaka 1988 mjini Mtwara na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi Naliendele na baadae shule ya Sekondari ya wasichana Mtwara kabla ya kujiunga na chuo cha uandishi wa habari na utangazaji TIME cha jijini Dar es Salaam mwaka 2008.

Anapatikana katika kipindi cha “LIFE STYLE” jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana na kwa wale wapenzi wa muziki wa reggae huyu ndio mwenyewe, jumapili saa 10: hadi 12:00 jioni.

Malengo yake makuu ni kuvuma katika anga za kimataifa katika taaluma yake. Mchukulie kama alivyo!